Mechi yetu ya kwanza ya Ligi Kuu ya NBC katika Uwanja wa nyumbani dhidi ya Coastal Union imemalizika kwa kufanikiwa kupata ushindi wa bao moja.
Tulianza mchezo kwa kasi huku tukiliandama lango la Coastal na kutengeneza nafasi nyingi lakini wapinzani wetu walikuwa imara kwenye kuzuia.
Tulimiliki sehemu kubwa ya mchezo ambapo dakika 45 za kwanza wapinzani wetu Coastal hawakufanya shambulizi huku pia wakiwa hawajapiga shuti lolote langoni kwetu.
Kipindi cha pili tulirudi kwa kasi kutafuta bao la uongozi lakini Coastal ambao wote walikuwa nyuma walikuwa imara kuzuia mafuriko ya mashambulizi yetu.
Ismail Toure alitupatia bao kwanza kwa kichwa dakika ya 74 baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Anicet Oura.
Matokeo haya yanatufanya kufikisha alama 12 na kurejea kileleni mwa msimamo baada ya kucheza mechi nne na kushinda mechi zote.
X1: Kassali, Duchu (Nindi 79'), Chilambo, Toure, De Reuck, Maema Gueye, Morice (Oura 62'), Doumbia (Mpanzu 62') Chama (Loemba 88'), Makgalwa (Mgunda 79')
Walioonyeshwa kadi: Chilambo 53' Doumbia 59'
X1: Chuma, Maabad, Andrew, Laurent, Ally, Shiza (Farid 65'), Aidan, Saad, Matheo, Arafat (Ally Said 84') , Najim (Robert 65')
Walioonyeshwa kadi: Matheo 31'