Tumefanikiwa kuinasa saini ya mlinzi kijana wa kati Ibrahim Abbas Nindi kwa mkataba wa miaka mitatu.
Nindi (19) ni kijana wa Kitanzania mwenye uwezo mkubwa na uzoefu wa kucheza Ligi Kuu ya NBC na hiyo ni moja ya sababu iliyotuvutia.
Katika umri huo mdogo Nindi amecheza timu ya KMC ya Kinondoni kabla ya baadae kujiunga na Mashujaa FC ya Kigoma.
Nindi pia ni mchezaji wa timu ya Taifa ya Vijana ya Tanzania chini ya umri wa miaka 20 'Ngorongoro Heroes' na ni mmoja wa nyota anayetazamwa kuwa staa wa baadae.
Tayari Nindi amejiunga na kikosi na yupo jijini Mwanza akiwa tayari kwa mchezo wa kesho dhidi ya Pamba Jiji.