Simba Sports Club

Tumeibuka Kidedea Katika Dabi ya Mzizima

16 Sep 2026

Kikosi chetu kimefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 katika Dabi ya Mzizima dhidi ya Azam FC katika mchezo uliopigwa Uwanja wa Azam Complex Chamazi.

Mchezo ulianza kwa kasi ya kawaida huku timu zote zikisomana huku mbinu bora za kuzuia kwa makocha wote zikionekana kufanya kazi.

Hata hivyo katika dakika 45 zote za kipindi cha kwanza mashambulizi yakiwa machache pande zote mpira ukichezwa zaidi katikati ya uwanja.

Dakika ya 58 mlinzi wa kati, Fasika Idumba alijiunga katika jitihada za kuokoa mpira wa kichwa uliopigwa na Rushine De Reuck kufuatia mpira wa kona uliopigwa na Nathaniel Chilambo.

Clatous Chama alitupatia bao la pili dakika ya 69 kwa shuti kali akiwa ndani ya 18 baada ya kumalizia pasi kutoka kwa Libbase Gueye.

Advertisement

Ushindi huu unatufanya kufikisha alama 18 tuliendelea kusalia nafasi ya pili kwenye msimamo sawa na wanaongoza ligi tofauti ya mabao ya kufunga baada ya kucheza mechi sita.

Baada ya mchezo wa Ligi Kuu ya NBC itasimama kupisha mechi za kalenda ya FIFA kwa ajili timu za Taifa.

X1: Foba, Mwaikenda (Kibeku 88') Msindo, Idumba, Stanic, Himid (Kiswanya 88') Sillah (Molia 77'), Kipre Jr (Nado 62') Zidane (Sopu 77'), Feisal, Mubiru

Walioonyeshwa kadi: Feisal 42' Himid 50' Msindo 52' Kiswanya 94'

X1: Kassali, Chilambo, Mligo, Toure, De Reuck, Kagoma, Gueye, Maema (Morice 90+3'), Mpanzu (Doumbia 83'), Chama (Jabaar 83'), Oura (Makgalwa 90')

Walioonyeshwa kadi: Toure 36'