Simba Sports Club

Tumekabidhi Choo Shule ya Msingi Kambi ya Nyoka

9 Nov 2026

Menejimeti ya klabu kwa kushirikiana na Mo Dewji Foundation leo tumekabidhi choo katika Shule ya Msingi Kambi ya Nyoka wilaya ya Karatu mkoani Arusha.

Ujenzi huu umekuja baada ya kuona changamoto wanayopitia twanafunzi wa shule kutokana na uchakavu wa vyoo wanavyotumia tulivyopita wakati wa uzinduzi wa wiki ya Simba ambayo ilifanyika katika Hifadhi ya Taifa Ngorongoro.

Mjumbe wa Bodi, Seleman Haroub amesema tuliahidi kujenga choo na tumetimiza na leo tunakabidhi ili watoto wetu waendelee kutumia.

Meneja Habari na Mawasiliano, Ahmed Ally amesema baada ya upembuzi yakinifu kufanyika juu ya gharama na vifaa vinavyohitajika kwenye ujenzi huo wa choo ulianza Agosti 2, 2026 na leo umekamilika rasmi.

Advertisement

"Tulipita hapa mwezi Agosti na tukakuta hali mbaya tukaona lazima tuwasaidie wadogo zetu kwa kushirikia na Mo Dewji Foundation leo tumekuja kuzindua," amesema Ahmed.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Mo Dewji Foundation, Adila Isihaka amesema tunaendelea kuwafikia wananchi hasa wenye katika elimu na ustawi wa jamii.

Nae Mwalimu mkuu wa Shule ya Msingi Kambi ya Nyoka, Onest William Tesha ameushukuru Uongozi wa Simba kwa kushirikiana na Mo Dewji Foundation kwa msaada huo ambao umerejesha hamasa kwa wanafunzi.

"Kwa moyo wa dhati naishukuru Simba na Mo Dewji Foundation kwa ujenzi wa Choo hiki cha kisasa ambacho wanafunzi watajisikia fahari hasa ukilinganisha na kile walichokuwa wanatumia awali," amesema Mwalimu Tesha.