Kocha msaidizi wa Simba Queens, Abdul Nassir Ahmada amesema maandalizi ya mchezo wa kesho wa Ligi kuu ya Wanawake Tanzania (WPL) dhidi ya Mashujaa Queens.
Ahmada amesema ligi ya msimu huu imezidi kuwa ngumu na timu nyingi zimeimarika lakini tumejipanga kuhakikisha tunatetea ubingwa.
Akizungumza kuelekea mchezo wa kesho, Ahmada amesema wachezaji wote wapo kwenye hali nzuri na tutaingia uwanjani kwa lengo la kupambania alama tatu.
"Maandalizi ya mchezo yamekamilika, tunafahamu utakuwa mchezo mgumu lakini tumejiandaa na tupo tayari kupata ushindi," amesema Ahmada.
Nahodha wa timu hiyo, Fatuma Issa 'Fetty Densa' amesema wachezaji wapo tayari kufuata maelekezo watakaopewa na walimu ili kuisaidia timu kupata alama zote tatu.
"Kwa upande wetu kama wachezaji tupo tayari kupambana kwa dakika zote 90 ili kuiwezesha timu kupata ushindi. Tunafahamu haitakuwa rahisi lakini tupo tayari," amesema Fetty Densa'.