Kocha mkuu, Steve Barker amechaguliwa kocha Bora wa Ligi kuu ya NBC wa mwezi Oktoba.
Barker ameshinda tuzo baada ya kuwashinda Florent Ibenge wa Azam FC na Juma Mgunda wa Namungo ambao aliingia nao kinyang'angiro hicho.
Katika mwezi Oktoba Barker ametuwezesha kushinda mechi zote tatu za ligi tulizocheza ikiwa ni ushindi wa asilimia 100.
Kwa upande wa kiungo mshambuliaji Elie Mpanzu nae ametwaa tuzo ya mchezaji Bora wa mwezi Oktoba baada ya kuwapiku Idd Seleman Nado wa Azam na Nathaniel Chilambo.
Katika mwezi Oktoba, Mpanzu amecheza dakika 241 katika mechi tatu na kufunga mabao matatu.