Simba Sports Club

Queens yaendelea kutoa dozi

4 Nov 2026

Simba Queens imefanikiwa kuibuka na ushindi wa bao moja dhidi ya Fountain Gate Princess katika mchezo wa ligi kuu ya Wanawake Tanzania (WPL) uliopigwa Uwanja wa Jamhuri Dodoma.

Mchezo ulianza kwa kasi huku timu zote zikishambuliana kwa zamu na kutengeneza nafasi nyingi lakini ufanisi haukuwa mzuri.

Licha ya mashambulizi na kosa kosa za hapa na pale lakini matokeo hayakubadilika katika dakika zote 45 za kipindi cha kwanza.

Bao pekee kwenye mchezo wa leo lilifungwa na Felister Mauki dakika ya 60 baada ya kujifunga kwenye jitihada za kuzuia kuzuia mpira uliopigwa na Aisha Mnunka.

Advertisement

Kocha mkuu wa Simba Queens alifanya mabadiliko ya kuwatoa Senaf Demise na Zainah Nandede na kuwaingiza Kusamfula na Mabinti Camara.

Ushindi huu umeifanya Simba Queens kufikisha alama sita baada ya kushinda mechi zote mbili za kwanza.

Simba Queens itashuka tena dimbani Novemba 11 katika Uwanja wa Lake Tanganyika kuikabili Mashujaa Queens.