Mchezo wetu wa tatu wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Singida Black Stars uliopigwa Uwanja wa Airtel mkoani Singida umemalizika kwa ushindi wa mabao 2-1.
Clatous Chama alitupatia bao la kwanza dakika ya 12 kwa shuti kali ndani ya 18 baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Libbase Gueye.
Shekhan Ibrahim aliisawazishia Singida bao hilo dakika ya 23 baada ya kupokea pasi kutoka Jeancy Mboma.
Baada ya bao hilo tuliendelea kuwa na umiliki mzuri wa mchezo huku tukifika zaidi langoni mwa Singida lakini umakini wa kuzitumia nafasi tulizopata ukawa mdogo.
Rushine De Reuck alitupatia bao la pili kwa mkwaju wa penati dakika ya 63 baada ya mlinzi Ismail Toure kufanyiwa madhambi ndani ya 18.
Mlinzi wa kushoto Anthony Mligo alitolewa kwa kuonyeshwa kadi nyekundu dakika ya 84 baada ya kuchezea madhambi kiungo mshambuliaji, Yusuph Adam.
Ushindi huu unatufanya kukusanya alama zote tisa kwenye mechi tatu za Kanda ya Ziwa na kutufanya kupanda juu ya msimamo wa NBC.
Baada ya mchezo huu kikosi kitarejea Dar es Salaam kujiandaa na mchezo wa nne dhidi ya Coastal Union utakaopigwa Uwanja wa Uhuru Alhamisi ya Agosti 27.
X1: Metacha, Abdulmarik, Sowah (Simchimba 69'), Imoro, Mboma, Mwashinga (Henry), Ande, Shekhan (Chasambi 85'), Tanimu, Nzaou (Yusuph 69'), Keyekeh (Pipino 45')
Walioonyeshwa kadi: Mboma 32' Nzaou 52'
X1: Abel, Chilambo, Mligo, Toure, De Reuck, Maema, Gueye (Doumbia 85'), Morice (Makgalwa 74'), Mpanzu (Nashon 90') Chama, Oura
Walioonyeshwa kadi: Mligo kadi nyekundu 84'