Leo saa 12 jioni kikosi chetu kitashuka katika Uwanja wa Airtel mkoani Singida kuikabili Singida Black Stars katika mchezo wa tatu wa Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2026/2027.
Kocha Mkuu, Steve Barker amefanya mabadiliko ya mchezaji mmoja ukilinganisha na kikosi kilichoanza mechi iliyopita dhidi ya Pamba Jiji.
Barker amemuanzisha kiungo mshambuliaji Morice Abraham kuchukua nafasi ya Ibraheem Jabaar ambaye anatumikia adhabu ya kadi nyekundu.
Hiki hapa kikosi kamili kilichopangwa:
Hussein Abel (28), Nathaniel Chilambo (26), Anthony Mligo (5), Ismail Toure (25), Rushine De Reuck (23), Neo Maema (35), Libbase Gueye (7), Clatous Chama (17), Elie Mpanzu (34), Morice Abraham (18), Anicet Oura (20).
Wachezaji wa Akiba:
Alexander Erasto(42), Vedastus Masinde (4), Ibrahim Nindi (16), Inno Loemba (10), Daud Semfuko (37), Ibrahim Doumbia (29), Ismail Mgunda (66), Kelvin Nashon (24), Keletso Makgalwa (11).