Mchezo wetu wa kwanza wa Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2025/2026 dhidi ya Kagera Sugar uliopigwa Uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera umemalizika kwa ushindi wa mabao 2-0.
Mchezo ulianza kwa kasi huku timu zote zikishambuliana kwa zamu kukiwa hakuna aliyebaki nyuma lakini mechi ikichezwa zaidi katikati ya uwanja.
Mlinzi wa kati, Ismail Toure alitupatia bao la kwanza kwa kichwa dakika ya 45 baada ya kumalizia mpira wa kona uliopigwa na Libasse Gueye.
Mlinzi wa kulia, David Kameta 'Duchu' alitolewa uwanjani dakika 55 baada ya kuonyeshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja kufuatia kumfanyia madhambi David Luhende.
Elie Mpanzu alitupatia bao la pili dakika ya 69 baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Libbase.
Mchezo wetu wa pili utakakuwa Jumatano Agosti 19 dhidi ya Pamba Jiji utakaopigwa saa 10 jioni Uwanja CCM Kirumba jijini Mwanza.
X1: Kipao, Dante, Salehe, Evastus, Mhilu (Yusuph 84') Milandu, Tangalo, Mudathir, Mwatelema (Jesto 59') Feka, Luhende (Nyenyezi 68')
Walioonyeshwa kadi: Dante 59'
X1: Kassali (Abel 85'), Duchu, Kibabage, Toure, De Reuck, Kagoma (Maema 45'), Gueye (Msimu 74') Jabaar, Doumbia (Mpanzu 62'), Morice (Chilambo 61'), Oura
Walioonyeshwa kadi: Duchu Kadi nyekundu 55'