Kikosi chetu kimeondoka kuelekea mkoani Kagera tayari kwa mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2026/2027 dhidi ya Kagera Sugar.
Mchezo huo ambao tunataraji utakuwa mgumu kutokana na ubora wa wapinzani wetu utapigwa kesho saa 10 jioni katika Uwanja wa Kaitaba.
Tumeondoka na kikosi cha wachezaji 26 tayari kwa mchezo ambao malengo yetu ni kupata alama tatu ili kuanza vema msimu mpya.
Wachezaji wote wamefanya mazoezi jana katika uwanja wetu wa Mo Simba Arena na hakuna aliyepata maumivu na leo jioni watafanya mazoezi ya mwisho kabla ya kesho kushuka dimbani.