Simba Sports Club

Queens yaendeleza wimbi la ushindi WPL

11 Nov 2026


Simba Queens imekuwa na mwendelezo mzuri kwenye ligi ya Wanawake baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mashujaa Queens katika mchezo uliopigwa Uwanja wa Meja Jenerali Mzee.

Mchezo ulianza kwa kasi huku timu zikishambuliana kwa zamu ambapo nafasi nyingi zilitengenzwa ingawa hazikuweza kutumiwa kwa ufanisi.

Nahodha, Vivian Corazone alitupatia bao la kwanza dakika ya 43 baada ya kuwazidi ujanja walinzi wa Mashujaa.

Advertisement

Zainah Nandede alitupatia bao la pili kwa kichwa dakika ya mwisho ya mchezo baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Fasila Adhiambo.

Kocha wa viungo Sibususo Makhula ambaye ndiye aliyeiongoza timu amefanya mabadiliko ya kuwatoa Asha Omary, Senaf Damise na Aisha Mnunka na kuwaingiza Brice Zanga, Zainah Nandede na Mabinty Camara.

Mchezo huu ni watatu tukiwa tumeshinda mechi zote tukiwa na alama tisa bila kuruhusu bao.

Simba Queens itashuka tena dimbani, Novemba 18 katika Uwanja wa KMC Complex kuikabili Ceasia Queens.