Simba Sports Club

Hivi hapa Viingilio mchezo dhidi ya FC 15 De Agosto

22 Oct 2026

Meneja Habari na Mawasiliano wa klabu, Ahmed Ally ametangaza rasmi viingilio vya mchezo wetu wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya FC 15 De Agosto utakaopigwa Jumapili katika Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam saa 10 jioni.

Ahmed amesema pamoja nakuwa tumepata ushindi mnono wa mabao mengi kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza lakini bado hatujamaliza na tunahitaji mashabiki wetu ili kuweka historia barani Afrika.

Ahmed amesema tunataka kuufanya mchezo wa Jumapili kuwa kama Simba Day namba mbili ambapo kwa sasa ni wazi tupo hatua nyingi kabla ya kuingia makundi hivyo ni siku ya kufurahi.

"Tunaongoza kwa mabao 6-1 ingawa kwenye mpira kuwa matokeo ya kushangaza lakini 15 De Agosto hawana uwezo wa kupindua meza Kibabe ndio maana tunatakiwa kuujaza Uwanja ili kuwarahisishia kazi wachezaji," amesema Ahmed.

Hivi hapa Viingilio:

Advertisement

Mzunguko Shilingi 5000

VIP Shilingi 30,000

Platinum Shilingi 150,000

Watakaonunua tiketi za Platinum watapata usafiri wa kutoka hotelini mpaka Uwanjani, watapewa eneo maalum, watapata chakula pamoja na vinywaji.