Simba Sports Club

Timu yafanya mazoezi kujiandaa Jamus Jumanne

26 Jul 2026

Baada ya mchezo wa jana wa Kombe la Kagame dhidi ya Mogadishu City leo kikosi kimefanya mazoezi ya utimamu pamoja na kuendelea na program ya kocha mkuu, Steve Barker.

Pamoja na mazoezi ya utimamu wa mwili pia kocha, Barker ameyatumia mazoezi hayo kama sehemu ya maandalizi ya mchezo wa pili wa Kundi B dhidi ya Jamus kutoka Sudan Kusini utakaopigwa Jumanne.

Mpaka sasa nyota wetu wote wamewasili nchini Rwanda kuendelea na maandalizi ya msimu mpya wa mashindano pamoja na kushiriki michuano ya CECAFA Kagame Cup inayoendelea.

Advertisement

Libbase Gueye ambaye alichelewa kujiunga na wenzake kutokana na changamoto ya kifamilia nae ameshiriki mazoezi hayo mwanzo mpaka mwisho na yupo tayari kwa ajili ya mechi ya Jumanne.

Katika mchezo wa Jumanne dhidi ya Jamus kocha, Barker atakuwa na machaguo mengi katika upangaji wa kikosi kwasababu wachezaji wote wamewasili nchini Rwanda