Simba Sports Club

Ibraheem Jabaar ni Mnyama

25 Jul 2026

Tumeinasa saini ya kiungo fundi Ibraheem Jabaar kutoka Stellenbosch FC ya Afrika Kusini kwa mkataba wa miaka miwili.

Jabaar raia wa Nigeria (24) anayefahamika kwa jina la utani la 'Messi wa Ankara' anaweza kucheza kama kiungo mkabaji namba sita, namba nane na pia winga zote.

Pamoja na ustadi wake wa kuzuia na kusifika kutengeneza uwiano kwenye timu, Jabaar ana uwezo mkubwa wa kufunga ambapo msimu uliopita amefunga mabao matatu na kusaidia kupatikana kwa mengine matano.

Advertisement

Jabaar pia amewahi kucheza katika timu ya Maccabi Petah Tikva ya Israel kabla ya kurejea tena Stellenbosch.

Msimu wa 2021/2022 Jabaar alitwaa tuzo ya mchezaji Bora wa mwaka kijana wa timu ya Stellenbosch.

Jabaar anakumbukwa kwa kuwepo kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Nigeria kulichoshiriki michuano ya AFCON chini ya umri wa miaka 17 ambayo iliyofanyika nchini Tanzania mwaka 2019.