Simba Sports Club

Karibu Simba Queens Senaf Demise

27 Jul 2026

Mshambuliaji nyota, Senaf Demise amejiunga na kikosi chetu cha Simba Queens kutoka Defence Mechal Sport Club ya Ethiopia baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili.

Senaf ni moja ya usajili ambao umebeba matumaini makubwa ya Simba Queens kuelekea msimu ujao wa mashindano 2026/2027.

Advertisement

Senaf pamoja nakuwa ni mshambuliaji lakini ana uwezo mkubwa wa kushuka chini kuchukua mipira na kuchezesha timu.

Senaf ametua nchini kujiunga na Simba Queens na tayari yupo kambini kujiandaa na michuano ya CECAFA itakayofanyika nchini Rwanda baadae mwezi ujao.