Simba Sports Club

Karibu Simba Ibrahim Doumbia

24 Jul 2026

Tumefanikiwa kuinasa saini ya mshambuliaji, Ibrahim Doumbia kutoka AS Korofina ya Mali kwa mkataba wa miaka miwili.

Doumbia raia wa Mali (19) ni mshambuliaji kijana mwenye uwezo mkubwa wa kufunga mabao kwa aina zote akitokea sehemu yoyote uwanjani.

Msimu uliopita akiwa na AS Korofina, Doumbia ameibuka mfungaji bora wa Ligi Kuu ya Mali akifunga mabao 17 na kusaidia kupatikana kwa mengine matano.

Advertisement

Doumbia ambaye amejuimuishwa pia kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Mali chini ya umri wa miaka 20 amefunga mabao 22 kwenye michuano yote baada ya kucheza mechi 26.

Malengo yetu ni kufanya vizuri kwenye michuano ya ndani pamoja na Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao na usajili tunaofanya imezingatia matakwa hayo.