Kikosi chetu kimefanya mazoezi asubuhi katika Uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera baada ya mchezo wa jana dhidi ya Kagera Sugar.
Wachezaji wote wameshiriki mazoezi hayo isipokuwa mlinda mlango Djibrilla Kassali ambaye alipata maumivu ya goti kwenye mchezo wa jana.
Baada ya mazoezi hayo kikosi kimeanza safari ya kuelekea jijini Mwanza tayari kwa mchezo wa pili wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Pamba Jiji utakaopigwa Jumatano saa 10 jioni Uwanja wa CCM Kirumba.
Timu itakapofika Mwanza wachezaji watapumzika na kesho jioni watafanya mazoezi ya mwisho kabla ya Jumatano kushuka dimbani.