Kikosi chetu kimefanya mazoezi katika Uwanja wa Gymkhana kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Yanga utakaopigwa siku ya Jumamosi.
Wachezaji wote wameshiriki mazoezi hayo na wapo kwenye hali nzuri na morali zao ziko juu kuelekea mtanange huo.
Nyota wetu Morice Abraham, Nathaniel Chilambo, Anthony Mligo na Inno Jospin Loemba ambao walikuwa kwenye majukumu ya timu zao za Taifa tayari wamejiunga na wameshiriki mazoezi hayo.
Nahodha, Shomari Kapombe ambaye alipata maumivu ya bega Agosti mwaka huu kwenye michuano ya CECAFA Kagame Cup nae ameshiriki mazoezi hayo mwanzo mwisho tayari kwa mchezo huo wa Dabi ya Kariakoo.