Baada ya mazoezi ya jioni ya leo yatakayofanyika katika Uwanja wetu wa Mo Simba Arena kikosi kitaingia moja kwa moja kambini kujiandaa na mchezo ujao wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Geita Gold.
Mchezo dhidi ya Geita Gold utapigwa Jumatatu, Agosti 31 katika Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo saa 12 jioni.
Wachezaji wote wataingia kambini kujiandaa na mchezo huo ambao tunafahamu utakuwa mgumu lakini tumejiandaa kupambana kuhakikisha ushindi unapatikana.
Tayari Viingilio vya mchezo huo vimetangazwa ambavyo ni Shilingi 5000 kwa mzunguko na Shilingi 10,000 kwa VIP.