Tamasha letu la Simba Day tayari linaendelea katika Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam na shamra shamra huku mashabiki wakijitokeza kwa wingi.
Pamoja na burudani mbalimbali zinazoendelea lakini tayari kumepigwa mechi tatu za mwanzo.
Mchezo wa kwanza ulikuwa kati ya Simba U17 dhidi ya Nkimi FC ambao ulimalizika kwa sare ya kufungana mabao 2-2.
Advertisement
Mchezo wa pili ulikuwa kati ya Menejimenti ambayo tumeibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Equity Bank.
Mchezo wa tatu ulikuwa kati ya Simba Veterans dhidi ya KT ambao umemalizika maveterani wameibuka na ushindi wa mabao 4-1.
Nyota wazamani kama nahodha John Bocco, Emmanuel Okwi, Medie Kagere, Mwinyi Kazimamoto, Victor Costa, Mustapha Hoza ni miongoni mwa nyota waliocheza kwa upande wa Veterans.