Awali mchezo huo ambao huvuta hisia za mashabiki wengi ndani na nje ya nchi ulipangwa kupigwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Mei 3 saa 11 jioni.
TPLB imetoa sababu ya mabadiliko ya uwanja ni kutokana na dimba la Benjamin Mkapa kufungwa kwa ajili ya matengenezo makubwa ikiwa ni maandalizi ya michuano ya AFCON 2027 Tanzania ikiwa ni muuandaji mwenza.
Advertisement
Sisi ambao ni wenyeji wa mchezo tayari tumepata taarifa juu ya mabadiliko hayo ya uwanja na mara timu itakaporejea kutoka Zanzibar itaendelea na maandalizi ya mchezo huo.