Kikosi cha wachezaji 22 kimeondoka nchini kuelekea Lilongwe Malawi tayari kwa mchezo wa kwanza wa hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Mighty Wonderers utakaopigwa siku ya Jumapili.
Meneja Habari na Mawasiliano, Ahmed Ally amesema kikosi kimeondoka jijini Dar es Salaam na kitaenda moja kwa moja Lilongwe.
Ahmed amesema maandalizi ya mchezo huo yamekamilika na wachezaji wote 22 waliosafiri wapo tayari kuhakikisha wanapambana kuisaidia timu kupata matokeo chanya.
Aidha, Ahmed ameweka wazi kuwa pamoja nakuwa tunaenda kukutana na timu bora ambayo ni Mabingwa wa nchi ya Malawi lakini Simba ni kubwa zaidi yao na tutaingia uwanjani kwa lengo la kutafuta ushindi.
"Timu yetu imeondoka kuelekea Malawi tayari kwa mchezo dhidi ya Mighty Wonderers utakaopigwa Jumapili, tunafahamu itakuwa mechi ngumu lakini tupo tayari kuwakabili," amesema Ahmed.