Simba Sports Club
News

Kocha Barker afunguka malengo ya Muungano

22 Apr 2026

Barker amesema Simba ni timu kubwa na michuano yoyote inayoshiriki lengo la kwanza ni kuchukua ubingwa na ndicho kilichotupeleka Zanzibar.

Kuhusu mchezo wa kesho dhidi ya Mafunzo, Barker amesema maandalizi yamekamilika kwa asilimia kubwa na leo kikosi kitafanya mazoezi ya mwisho.

"Lengo la kwanza la Simba kwenye kila mashindano inayoshiriki ni kutwaa ubingwa ndio maana tupo hapa, tunafahamu michuano hii itakuwa migumu lakini tumejipanga," amesema Barker.

Advertisement

Kwa upande wake nahodha wa timu, Shomari Kapombe ameunga mkono kauli ya Kocha Barker kuwa kila mchezaji anafahamu kuwa tunahitaji kushinda taji la michuano hii.

Kapombe amesema hata wachezaji wageni waliokuja wamewaambia umuhimu wa kujituma ili kuweza kufikia malengo ambayo mara zote klabu imejiwekea ya kutwaa ubingwa.

"Tupo tayari kwa michuano ya Kombe la Muungano, tunafahamu Mafunzo watatupa upinzani mkubwa na tunawaheshimu. Tumekuja mara nyingi hapa na tunafahamu haitakuwa rahisi lakini tupo tayari," amesema Kapombe.

Back to homepage
Share this story