Simba Sports Club

Kauli ya Kocha kuelekea mchezo dhidi ya Polisi Kenya

7 Aug 2026

Kocha mkuu, Steve Barker amesema kikosi chetu kipo kwenye hali nzuri kuelekea mchezo wa kesho wa kirafiki wa Kimataifa dhidi ya Polisi Kenya kwenye Tamasha la Simba Day utakaopigwa Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Barker amesema wachezaji wote wapo kwenye hali na wapo tayari kujitoa muda wote kuhakikisha wanawapa furaha Wanasimba ambao anaamini watakuja kwa wingi.

Barker ameongeza kuwa pamoja nakuwa ni mchezo wa kirafiki lakini tutacheza kwa asilimia 100 ili kuwaonyesha mashabiki wetu timu yao kuelekea msimu mpya wa mashindano 2025/2026.

"Tupo tayari kwa Simba Day, tumecheza mechi nne nchini Rwanda, na wachezaji wameonyesha uwezo mkubwa na mpaka kufikia leo naweza kusema wapo tayari kwa mchezo wa kesho," amesema Barker.

Advertisement

Kwa upande wake, mlinzi wa kulia, David Kameta 'Duchu' amewaomba Wanasimba wajitokeze kwa wingi kesho ili kuja kuona timu yao ambayo watakuwa nayo kwa msimu mzima.

Duchu amesema mara zote mashabiki wamekuwa upande wetu na hawajawahi kutuacha na anaamini hata kesho kuelekea watakuja kwa wingi kama kawaida yao.

"Sisi kama wachezaji tupo tayari kwa mchezo wa kesho, wachezaji wapya wamekuja na wameongeza kitu kikubwa kikubwa Wanasimba mje kwa wingi Uwanja wa Uhuru kesho kushuhudia Simba Day," amesema Duchu.