Simba Sports Club

Kauli ya Kocha Barker kuelekea mchezo dhidi ya Mashujaa

12 Oct 2026

Kocha mkuu, Steve Barker amesema maandalizi ya mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Mashujaa yanaendelea vizuri na wachezaji wote wapo kwenye hali nzuri.

Barker amesema baada ya mchezo wa Dabi jana wachezaji wamefanya mazoezi na wapo tayari kwa ajili ya mechi na tunafahamu itakuwa mechi ngumu.

Barker ameongeza kuwa Mashujaa ni timu imara na ina kocha mzuri na msimu uliopita walitupa changamoto lakini tumejiandaa na tupo tayari kwa mchezo.

Advertisement

"Maandalizi ya mchezo yamekamilika, tunataraji kupata upinzani mkubwa kutoka kwa Mashujaa. Tunakumbuka msimu uliopita walitupa changamoto kubwa lakini tumejipanga na tutaingia katika mchezo tukiwa na lengo la ushindi," amesema Barker.

Akizungumza kwa niaba ya wachezaji mlinzi wa kushoto, Anthony Mligo amesema kila kitu kimekamilika na morali ipo juu tayari na lengo ni kupata ushindi.

"Kama wachezaji tumejiandaa vizuri na tupo tayari kupokea maelekezo kutoka kwa makocha wetu ili kuendelea kupata alama tatu. Tunawaheshimu Mashujaa wana timu nzuri na benchi bora la ufundi lakini kwetu tupo tayari na lengo ni kuhakikisha tupata ushindi," amesema Mligo.