Tumefanikiwa kuinasa saini ya mshambuliaji, Mabinty Camara kutoka Determine Girls ya Liberia kwa mkataba wa miaka miwili.
Mabinty raia wa Guinea ni mchezaji mzuri ambaye moja ya sifa yake kubwa ni ustadi wa kufunga mabao pamoja na kutengeneza nafasi kwa wengine.
Advertisement
Kuelekea msimu mpya wa mashindano 2026/2027 tumejipanga kuhakikisha tunakisuka kikosi chetu ili kuweza kutetea taji letu la Ligi pamoja na kufanya vizuri kimataifa.
Mabinty ametua nchini kujiunga na Simba Queens na tayari yupo kambini kujiandaa na michuano ya CECAFA itakayofanyika nchini Rwanda baadae mwezi ujao.