Mshambuliaji, Kusamfula Musakanda Rida amejiunga na Simba Queens kuelekea msimu mpya wa mashindano 2026/2027 kwa mkataba wa miaka miwili.
Kusamfula ni mshambuliaji raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambaye tumemsajili kutoka CSF Bikira ya nchini humo.
Advertisement
Kusamfula ni mchezaji mwenye uwezo wa michuano ya Afrika na tunataraji atakuwa muhimili mkubwa wa Queens kuelekea msimu ujao.
Kusamfula tayari amejiunga na kikosi cha Simba Queens kinachojiandaa na michuano ya CECAFA ambayo itafanyika nchini Rwanda mwezi ujao