Barker amesema timu ambazo hazipo kwenye nafasi nzuri kwenye msimamo mara nyingi zikikutana na timu kubwa zinapambana kujikwamua kitu ambacho kinaongeza ugumu wa mchezo.
Barker ameongeza kuwa tutaingia kwenye mchezo huo tukiwa na malengo ya kuendelea kutandaza soka safi na kupata alama tatu.
Akizungumzia hali ya kikosi kocha, Barker amesema tutawakosa, Shomari Kapombe na Yusuph Kagoma ambao wanatumikia adhabu ya kadi tatu za njano lakini wengine wote wapo tayari kwa mchezo.
"Utakuwa mchezo mgumu na hatutaidharau hata kidogo Fountain Gate kwakuwa ipo chini kwenye msimamo bali tutaingia kwa tahadhari zote ili tupate alama tatu," amesema Barker
Akizungumza kwa niaba ya wachezaji wenzake mshambuliaji, Seleman Mwalimu amesema maandalizi yamekamilika na wote wapo tayari kwa mchezo.
Mwalimu amesema kila mmoja anafahamu umuhimu wa kupata alama tatu kwenye mchezo huo ingawa tunafahamu utakuwa mgumu.
"Sisi kama wachezaji tupo tayari kwa mchezo ambao tunafamu utakuwa mgumu lakini tumejiandaa kupata alama tatu tatu," amesema Mwalimu.