Simba Sports Club

Alichosema kocha Barker kuelekea mchezo dhidi ya Pamba

18 Aug 2026

Kocha mkuu, Steve Barker amesema maandalizi ya mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Pamba Jiji utakaopigwa Uwanja wa CCM Kirumba saa 10 jioni yamekamilika.

Barker amesema wachezaji wapo kwenye hali nzuri na tumejiandaa kuhakikisha tunapata alama tatu na kuendelea kuwa kubaki katika nafasi za juu kwenye msimamo.

Barker ameongeza kuwa haitakuwa mechi rahisi kutokana na ubora walionao wapinzani wetu hasa ukizingatia tunacheza ugenini lakini hata hivyo tumejipanga kuwakabili.

Advertisement

"Tunafahamu tunaenda kukutana na mpinzani mgumu ambaye yupo nyumbani lakini malengo yetu ni kuendelea kupata ushindi ili kukaa katika nafasi za juu ili kuongeza hali ya kujiamini kikosi," amesema Kocha Barker.

Akizungumza kwa niaba ya wachezaji kiungo mkabaji, Kelvin Nashon amesema kila kitu pamoja na ugumu na ubora walionao Pamba sisi tumejipanga kuhakikisha tunashinda na kupata alama tatu ugenini.

"Kwa maandalizi tuliyonayo sisi kama Simba tuna kila sifa na sababu ya kupata ushindi katika mchezo wa kesho dhidi ya Pamba Jiji ingawa tunajua tunaenda kukutana na timu ngumu lakini tuna wachezaji wenye ubora mkubwa ambao wanaweza kufanya lolote," amesema Nashon.