Mgunda: Tuna mechi ngumu kesho

Kaimu Kocha Mkuu Juma Mgunda amesema maandalizi ya mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Azam FC yamekamilika.

Mgunda amesema wachezaji wapo kwenye hali nzuri huku akikiri utakuwa mchezo mgumu kutokana na ubora wa Azam lakini tupo tayari kuwakabili.

Mgunda ameongeza kuwa Azam ni timu bora na ndio maana ipo nafasi ya pili kwenye msimamo lakini tumejipanga kuhakikisha tunashindana na kushinda.

“Itakuwa mechi nzuri, Azam ni timu bora lakini tumejipanga kucheza na timu bora na tupo tayari kupambana ili kupata ushindi.”

“Maandalizi ya mchezo yamekamilika, wachezaji wapo kwenye hali nzuri tayari kupambana na lengo letu ni kupata pointi tatu,” amesema Mgunda.

Kwa upande wake mlinzi wa kati Hussein Kazi amesema wachezaji wapo tayari kupigania timu ili kupata pointi tatu muhimu.

“Kwa upande wetu wachezaji tupo tayari kwa ajili ya mchezo wa kesho, tunajua itakuwa mechi ngumu lakini tumejipanga kuhakikisha tunashinda,” amesema Kazi.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER