Tumezipata pointi zote tatu Jamhuri Dodoma

Mchezo wetu wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Dodoma Jiji uliopangwa Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma umemalizika kwa kuibuka na ushindi wa bao moja.

Mchezo huo ulikuwa mkali muda wote huku zikishambuliana kwa zamu lakini umakini katika eneo la mwisho ulichelewesha kupatikana kwa idadi kubwa ya mabao.

Mshambuliaji Freddy Michael alitupatia bao hilo pekee baada ya kupokea pasi safi jutoka kwa Edwin Balua na kupiga shuti lilomshinda mlinda mlango wa dodoma jiji Aaron kalambo.

Baada ya bao hilo tuliendelea kulishambulia lango la Dodoma huku nao wakija mara kadhaa kwetu lakini mlinda mlango, Hussein Abel alikuwa imara.

Kipindi cha pili tulirudi kwa kasi na kutafuta mabao zaidi lakini safu ya ulinzi ya Dodoma ilikuwa imara kuwadhibiti washambuliaji wetu.

Kocha Juma Mgunda alifanya mabadiliko ya kuwatoa Freddy Michael na Sadio Kanoute na kuwaingiza Pa Omar Jobe na Saido Ntibazonkiza.

Ushindi huu unatufanya kufikisha pointi 60 baada ya kucheza mechi 27 tukiendelea kubaki nafasi ya tatu.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER