Mashabiki 35,000 kuziona Simba, Arrows uwanjani

Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) limeruhusu mashabiki 35,000 kuingia uwanjani kushuhudia mchezo wetu wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Red Arrows utakaopigwa Jumapili katika Uwanja wa Benjamin Mkapa saa 10 jioni.

Uongozi wa klabu umepokea barua rasmi kutoka CAF ikiwa na maelekezo hayo ambayo tunapaswa kuyafuata.

CAF imekuwa na utaratibu wa kuruhusu idadi fulani ya mashabiki kuingia uwanjani kwa ajili ya kujikinga na janga la ugonjwa unaosababishwa na virusi vya corona (Covid-19).

Pamoja na mambo mengine, CAF imesisitiza kufuatwa kwa taratibu zote za kujikinga na ugonjwa huo kama kukaa kwa nafasi baina ya mtu na mtu na kuvaa barakoa kwa kila atakayehudhuria.

Tayari viingilio vya mchezo ambapo Mzunguko Sh 5,000, VIP B na C Sh 20,000 na VIP A Sh 40,000.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER