Manula afunguka siri ya kiwango chake kwa sasa

Mlinda mlango namba moja, Aishi Manula ametaja siri ya kiwango chake kwa sasa ni kutokana na ushirikiano mkubwa anaoupata kutoka kwenye safu ya ulinzi.

Manula amesema ushirikiano anaopata kutoka kwa Joash Onyango, Pascal Wawa, Mohammed Hussein na Shomari Kapombe ni mkubwa na ndiyo unaomfanya kuzidi kung’ara siku hadi siku.

Manula ameongeza kuwa wakati mwingine anawaelekeza walinzi wake kwa lugha kali (kuwafokea) ili kutimiza malengo ya kuhakikisha timu inafanya vizuri.

“Kiwango changu kinatokana na ushirikiano baina ya safu yetu ya ulinzi. Mabeki wamekuwa wakihakikisha sifikiwi kirahisi na ikitokea wamepitwa na mimi nasahihisha makosa yao,” amesema Manula.

Manula amesema kwa sasa malengo yake ni kuhakikisha anaisaidia timu kutetea ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom, kufikia malengo ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika na kwenda kucheza soka la kulipwa nje ya nchi.

Mlinda mlango huyo amecheza mechi 13 bila kuruhusu bao (clean sheet) akiwa anaongoza miongoni mwa makipa wote wanaoshiriki Ligi Kuu.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

  1. Nimefurahi sana simba sc kuingia robo finali
    Ooooooooooooooooooooooooooooooooh
    TUNAOMBA TUJUE RATIBA YA ROBO FINALI

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER