Kanoute akiri Ligi ya Tanzania ngumu, ataja Viwanja

Kiungo mkabaji Sadio Kanoute, amekiri Ligi Kuu ya Tanzania (TPL) ni ngumu kutokana na timu nyingi kucheza soka lenye matumizi makubwa ya nguvu.

Kanoute amezitazama mechi zetu mbili za ligi dhidi ya Biashara United na Dodoma Jiji na kusema matumizi ya nguvu ni makubwa hivyo si rahisi na inapaswa kujipanga vizuri ili kuimudu.

Kiungo huyo ameongeza kuwa changamoto nyingine aliyoiona kwenye ligi ni aina ya viwanja vinavyotumika hasa eneo la kuchezea (pitch) si rafiki na wakati mwingine timu ilazimika kubadili mfumo ili kuendana na mazingira.

“Nimepata nafasi ya kuziangalia mechi zetu za kwanza, kiukweli ligi ni ngumu sababu timu nyingi zinatumia nguvu kubwa na viwanja navyo si rafiki sana lakini tunapaswa kuyakabili mazingira,” amesema Kanoute.

Kanoute amerejea mazoezini jana baada ya kupona maumivu ya bega aliyopata katika mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga uliopigwa Septemba 25, Uwanja wa Benjamin Mkapa.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER