Gomes: Nitabaki kuwa shabiki mkubwa wa Simba

Aliyekuwa Kocha Mkuu Didier Gomes, amesema Simba itabaki moyoni mwake na ataendelea kuishabikia kutokana na ushirikiano mkubwa alioupata muda wote aliokuwapo.

Gomes amesema ataendelea kuiunga mkono timu katika michuano yote na anaitakia kila la kheri katika maisha mapya bila yeye.

Gomes pia amemshukuru Mwekezaji Mohamed Dewji ‘Mo’ kwa ukishiriakiano mkubwa aliompa, Mtendaji Mkuu Barbara Gonzalez, wachezaji, benchi la ufundi na mashabiki kwa sapoti kubwa waliyompa.

“Napaswa kuwajibika kwa matokeo ya Jumapili, tayari tulikuwa mbele kwa mabao matatu wakati tumebakiwa na dakika 45 tu lakini kitendo cha wapinzani kusawazisha na kututoa ni suala lisilovumilika na nimeamua kuwajibika.

“Simba inabaki kuwa familia yangu, tumepata mataji mawili pamoja,vla ligi kuu na Azam Sports Federation Cup, kwa ukaribu na maisha tuliyoishi nabaki kuwa shabiki namba moja na ninaitakia kila la heri,” amesema Gomes.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER