Mgunda: Tulicheza kwa kufuata maelekezo

Kocha Mkuu, Juma Mgunda amesema licha ya ushindi wa mabao 2-0 tuliopata dhidi ya Mtibwa Sugar mechi haikuwa rahisi lakini lakini wachezaji walicheza huku wakifuata maelekezo.

Mgunda amesema ukiangalia nafasi iliyopo Mtibwa na kiwango wanachoonyesha uwanjani ni vitu viwili tofauti na walitupa mechi ngumu.

Mgunda ameongeza kuwa wachezaji walifuata maelekezo aliyowapa na ndio maana sababu ya ushindi huo na sasa tunajipanga kwa mchezo unaofuata.

“Haikuwa rahisi, nasi tulijipanga kwa ajili ya mechi hii. Mtibwa ni timu nzuri, ina wachezaji na kocha bora na tunafahamiana lakini tulihakikisha tunatumia vizuri nafasi tulizotengeneza.”

“Pamoja na ushindi huu lakini kuna mazuri yalikuwepo na mapungufu pia tunaenda kujipanga mazoezini kwa ajili ya mchezo ujao,” amemaliza Mgunda.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER