Mgunda: Maandalizi dhidi ya Tabora yamekamilika

Kocha Mkuu Juma Mgunda amesema maandalizi ya mchezo wetu wa kesho wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Tabora United utakaopigwa Uwanja wa Azam Complex saa 12:15 jioni yamekamilika.

Mgunda amesema wachezaji wapo kwenye hali nzuri tayari kupambana kwa ajili ya kupata matokeo ya ushindi ingawa haitakuwa mechi rahisi.

Mgunda ameongeza tutaingia kwenye mchezo wa kesho tukiwa tunafahamu tunacheza na timu ambayo ipo kwenye ligi kama sisi bila kujalisha ipo kwenye nafasi gani lakini hatuwadharau.

“Tupo tayari kwa mchezo wa kesho dhidi ya Tabora, hata hapa nimetoka mazoezini wachezaji wapo kwenye hali nzuri. Lengo letu ni kuhakikisha tunashinda kila mchezo.

“Tunaenda kupambana na Tabora tukiwa tunajua haipo kwenye nafasi nzuri lakini huu ni mpira hatuwezi kuwadharau, tutaingia kwa tahadhari zote lakini tunahitaji kushinda mchezo,” amesema Mgunda.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER