Zoran: Sina presha kufanya kazi Simba

Kocha wetu mpya Zoran Maki amekiri Simba ni timu kubwa lakini hana presha kuiongoza kwani amefanya kazi katika Bara la Afrika kwa miaka sita.

Zoran amesema amechukua ubingwa nchini Algeria na CR Belouzdad na ameshiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika pamoja na Shirikisho hivyo anaamini anaweza kufanya hivyo akiwa hapa.

Kuhusu muda wa maandalizi kuelekea msimu mpya wa ligi Zoran amesema itamtosha kukiandaa kikosi na kurejesha ubora wake wa kupambania mataji.

Kuhusu usajili Zoran amesema ameshirikishwa katika kusajili wachezaji wapya na anaamini tutakuwa na timu imara yenye kuleta ushindani ndani na michuano ya Afrika.

“Simba ni timu kubwa ina mashabiki wengi. Nina uzoefu wa mazingira ya Afrika, hata huu muda wa mwaka mmoja naweza kufanya mambo makubwa,” amesema Zoran.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER