Kikosi kitakachotuwakilisha dhidi ya Mashujaa

Kikosi chetu leo saa 10 jioni kitashuka katika Uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma kuikabili Mashujaa FC katika mchezo wa hatua ya 16 bora ya michuano ya CRDB Bank Federation Cup.

Kocha Abdelhak Benchikha amefanya mabadiliko ya wachezaji wanne ukilinganisha na kikosi kilianza dhidi ya Al Ahly kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Benchikha amewaanzisha Ally Salim, Israel Patrick, Kennedy Juma na Pa Omar Jobe kuchukua nafasi za Ayoub Lakred, Shomari Kapombe, Henock Inonga na Sadio Kanoute.

Hiki hapa Kikosi kilichopangwa:

Ally Salim (1), Israel Patrick (5), Mohamed Hussein (15), Kennedy Juma (26), Che Malone (20), Babacar Sarr (33), Kibu Denis (38), Fabrice Ngoma (6), Pa Omar Jobe (18), Said Ntibazonkiza (10), Clatous Chama (17).

Wachezaji wa Akiba:

Hussein Abel, David Kameta (3), Shomari Kapombe (15), Hussein Kazi (16), Mzamiru Yassin (19), Sadio Kanoute (8), Ladaki Chasambi (36), Willy Onana (7), Freddy Michael (18).

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER