Tumegawana Pointi Na Namungo Ruangwa

Mchezo wetu wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Namungo FC uliopigwa Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa Mkoani Lindi umemalizika kwa sare ya kufungana mabao 2-2.

Kiungo mshambuliaji Kibu Denis alishindwa kuendelea na mchezo baada ya kufanyiwa madhambi na Hamis Halifa na kutolewa dakika ya 28 nafasi yake ukachukuliwa na Pa Omar Jobe.

Willy Onana alitupatia bao la kwanza dakika ya 34 kwa shuti kali nje kidogo ya 18 baada ya kuwazidi ujanja walinzi wa Namungo kufuatia kupokea pasi kutoka kwa Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr’.

Namungo walisawazisha bao hilo dakika ya 39 kupitia kwa Kelvin Sabato kwa kichwa akimalizia mpira wa adhabu uliopigwa na Ayoub Semtawa.

Edwin Balua alitupatia bao la pili dakika ya 69 kwa mpira wa adhabu uliotinga wavuni moja kwa moja nje kidogo ya 18 kufuatia Abdallah Hamis amis kufanyiwa madhambi.

Namungo walisawazisha bao hilo dakika ya 90 baada ya mlinzi Kennedy Juma kujifunga katika jitihada za kukoa mpira wa krosi uliopigwa na Meddie Kagere.

Matokeo haya yanatufanya kufikisha pointi 47 tukiwa nafasi ya tatu kwenye msimamo baada ya kucheza mechi 22.

X1: Nahimana, Kibailo, Charles, Magingi, Mukombozi, Nyenye (Mwashinga 78′), Buswita, Domayo (Manyanya 78′), Sabato (Kagere 67′), Semtawa (Kabunda 67′), Masawe

Walioonyeshwa kadi: Nyenye 25′ Semtawa 37′

X1: Lakred, Israel Zimbwe Jr, Che Malone, Kennedy, Babacar (Hamis 45′), Onana, Fabrice Ngoma, Freddy, Kibu (Jobe 32′), Balua

Walioonyeshwa kadi: Zimbwe Jr 62′

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER