Kikosi chetu leo saa moja usiku kitashuka katika Uwanja wa Azam Complex Chamazi kuikabili Geita Gold kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya NBC.
Kocha Juma Mgunda amefanya mabadiliko ya wachezaji wawili ukilinganisha na kile kilichocheza dhidi ya Dodoma Jiji wiki iliyopita.
Hiki hapa kikosi kamili kilichopangwa:
Hussein Abel (30), Shomari Kapombe, Mohamed Hussein (15), Kennedy Juma (26), Che Malone (20), Fabrice Ngoma (6), Edwin Balua (37), Mzamiru Yassin (19), Pa Omar Jobe (2), Saido Ntibazonkiza (10), Ladaki (36).
Wachezaji wa Akiba:
Ayoub Lakred (40), David Kameta (3), Hussein Kazi (16), Abdallah Hamis (13), Babacar Sarr (33), Saleh Karabaka (23), Willy Onana (7), Sadio Kanoute (8).