Simba yapata alama muhimu ugenini

Sare ya bila kufungana dhidi ya Al Merreikh kwenye mchezo wa tatu wa Ligi ya Mabingwa Afrika imetupa alama moja muhimu na kutufanya kuendelea kusalia kileleni mwa kundi A.

Matokeo haya yanatufanya kufikisha alama saba ambazo haziwezi kufikiwa na Al Ahly pamoja na AS Vita wenye alama tatu kila mmoja na watakutana wenyewe baadae usiku.

Katika mchezo wa leo hatukutengeneza nafasi nyingi kama kawaida yetu inagwa tulimiliki sehemu kubwa ya mechi kwenye kila kipindi.

Katika mchezo wa leo Kocha, Didier Gomez aliwatoa Mzamiru Yassin, Rally Bwalya, Clatous Chama na Chris Mugalu nafasi zao zikachukuliwa na Erasto Nyoni, Hassan Dilunga, Francis Kahata na Medie Kagere.

Machi 16 tutacheza mechi ya marudinano na Merreikh katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER