Pablo abadili watano mbele ya Namungo leo

Kocha Mkuu Pablo Franco, amefanya mabadiliko ya wachezaji watano katika mchezo wa leo wa Ligi Kuu dhidi ya Namungo kulinganisha na kikosi kilichoanza mechi iliyopita dhidi ya Yanga.

Wachezaji hao ni Peter Banda, Mzamiru Yassin, Medie Kagere, Rally Bwalya na Kibu Denis ambao wamechukua nafasi za Pape Sakho, Chris Mugalu, Clatous Chama, Bernard Morrison na Sadio Kanoute.

Kagere ataongoza idara ya ushambuliaji akipata msaada wa karibu kutoka kwa viungo washambuliaji Banda, Bwalya na Kibu.

Kikosi Kamili kilivyopangwa

Aishi Manula (28), Shomari Kapombe (12), Mohamed Hussein (15), Joash Onyango (16), Henock Inonga (29), Jonas Mkude (20), Peter Banda (11), Mzamiru Yassin (19), Medie Kagere (14), Rally Bwalya (8), Kibu Denis (38).

Wachezaji wa Akiba

Beno Kakolanya (30), Israel Patrick (5), Gadiel Michael (2), Pascal Wawa (6), Erasto Nyoni (18), Pape Sakho (10), John Bocco (22), Yusuf Mhilu (27), Jimmyson Mwanuke (21)

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER