Simba Sports Club
News

Zungu akabidhi milioni 15 za bao la mama

22 Sep 2024

Mh. Zungu amesema lengo la Dkt. Samia kutoa pesa kwa kila bao linalofungwa kwa timu za Tanzania kwenye michuano ya Kimataifa ni kuongeza hamasa ili kufanya vizuri.

Zungu amesema Rais Samia ni mpenda michezo na anapenda kuona timu za Tanzania zikifanya vizuri kwenye michuano ya Kimataifa ndio maana anatoa pesa kwa ajili ya hamasa.

"Nichukue nafasi hii kuwapongeza wachezaji kwa kupigania timu na kufuzu hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho, na nipo hapa kuwakabidhi milioni 15 kutoka kwa Rais Samia na amefurahi kama Watanzania wengine," amesema Mh. Zungu.

Advertisement

Akizungumza kwa niaba ya wachezaji nahodha wa timu Mohamed Hussein 'Zimbwe Jr' amemshukuru Rais Samia kwa motisha hiyo anayotoa na pia amesema wataendelea kupambana mara zote.

"Kwanza tunamshukuru mama yetu kwa kutujali na kuthamini kazi yetu nasi tunamuahidi tutaendelea kufanya vizuri kwa ajili yake na kwetu pia," amesema Zimbwe Jr.

Back to homepage
Share this story