Baada ya kuwasili katika viwanja vya Zakhem kulipofanyika uzinduzi huo wanachama na wapenzi waliohudhuria walilipuka kwa furaha.
Zuchu ambaye anatokea katika Lebo kubwa ya Muziki nchini ya WCB chini ya Supastaa Diamond Platnum ametoa kionjo cha wimbo maalum atakaoimba siku hiyo.
Zuchu amewaomba Wanasimba kujitokeza kwa wingi uwanjani siku ya Jumatatu huku akiwaahidi kuwapagawisha kutokana na maandalizi anayoendelea nayo.
Advertisement
"Wanasimba wenzangu naomba tukutane kwa wingi kwa Mkapa, nawaahidi sitawaangusha nimewaandalia furaha ya kutosha," amesema Zuchu.
Mbali na Zuchu kutakuwa na burudani mbalimbali kutoka wa wasanii ambao tutaendelea kuwatangaza kuanzia kesho mpaka siku ya kilele.