Simba Sports Club
News

Zoran awavulia kofia wachezaji Misri

17 Jul 2022

Akizungumza na Simba App baada ya kumaliza mazoezi, Zoran amesema vijana wake wamezoeana kwa haraka hali inayompa matumaini ya kuendelea kutengeneza timu ya ushindani kuelekea msimu mpya wa ligi.

Kuhusu hali ya utimamu wa mwili Zoran amesema licha ya kuwa wachezaji wametoka kwenye mapumziko lakini utimamu wao wa mwili uko juu.

Akielezea program ya mazoezi katika kipindi chote cha Pre Season kocha Zoran amesema timu itakuwa ikifanya mazoezi mara mbili kwa siku na anataraji kucheza mechi nne au tano za kirafiki hapa Misri.

Advertisement

Jana Uongozi wa klabu ulimtambulisha Sbai Karim kama kocha wa viungo na kocha msaidizi ambapo Zoran amesema amefurahishwa na kocha huyo raia wa Tunisia kwani anamfahamu ubora wake na uwezo wake

'Naamini ujio wa Sbai utaenda kuongeza chachu ya mafanikio katika kikosi chetu, maendeleo ya wachezaji ni mazuri utimamu wao upo juu na unaniridhisha," amesema kocha Zoran.

Sbai anatajia kuwasili kesho hapa Misri tayari kuanza majukumu yake ndani ya kikosi chetu.

Back to homepage
Share this story