Simba Sports Club
News

Zoezi la hamasa lahitimishwa Temeke Stereo

6 Mar 2023

Zoezi letu limeanzia Uwanja wa Benjamin na kuelekea Mbagala ambapo njiani tulikuwa tunasimama kuuza tiketi za mchezo pamoja na jezi ambapo lilifikia tamati katika soko la Temeke Stereo.

Meneja Habari na Mawasiliano, Ahmed Ally amewasisitiza mashabiki kujitojeza kwa wingi uwanjani kesho kuipa sapoti timu na wasidhani itakuwa mechi rahisi kwakuwa tuliwafunga kwao.

"Kocha Mkuu Roberto Oliviera 'Robertinho' na wasaidizi wake wao wamemaliza kazi yao wachezaji wapo tayari tuliobaki ni sisi mashabiki kujitojeza kwa wingi uwanjani, nina imani kwa umoja wetu Vipers hatoki kesho kwa Mkapa," amesema Ahmed.

Advertisement

Ahmed amewasisitiza mashabiki wetu kununua tiketi mapema kwa wale ambao hawajanunua ili kuepeuka usumbufu ukizingatia mchezo wetu utapigwa saa moja usiku.

Jana zoezi la hamasa lilifanyika Coco Beach ambapo kulikuwa na shughuli mbalimbali za burudani zililoambatana na mechi za mpira wa miguu kwa wanaume na rede kwa wanawake.

Back to homepage
Share this story