Zimbwe Jr amesema benchi la ufundi pamoja na wachezaji wanafahamu umuhimu wa ushindi kwenye mchezo wa kesho ndio maana mapungufu yaliyotokea yamefanyiwa kazi.
Akizungumzia mchezo wenyewe Zimbwe Jr amesema utakuwa mgumu kwakuwa wenyeji Bravos wanahitaji alama tatu ili kufufua matumaini ya kufuzu robo fainali.
Advertisement
"Ni mechi muhimu kwetu kupata alama tatu kwakuwa zitatufanya kuwa tumefuzu moja kwa moja lakini kwa wenzetu itakuwa wameaga mashindano kwahiyo lazima itakuwa mechi ngumu."