Simba Sports Club
News

Zimbwe Jr awaita mashabiki kuimaliza Ihefu Kesho

9 Apr 2023

Zimbwe Jr amesema mashabiki wana mchango mkubwa huku akiwaahidi furaha baada ya dakika 90.

Zimbwe ameongeza kuwa mchezo utakuwa mgumu sababu tumetoka kuwafunga Ihefu kwenye michuano ya Azam Sports Federation siku mbili zilizopita hivyo watataka kulipa kisasi.

Advertisement

"Haitakuwa mechi rahisi Ihefu ni timu nzuri na jambo jingine litakalofanya mchezo kuwa mgumu ni kutokana tumetoka kuwafunga juzi kwahiyo na wao watataka kulipa kisasi.

"Kikubwa tunawaomba mashabiki wetu wajitokeze kwa wingi uwanjani kuja kutupa sapoti, sisi wachezaji tupo kamili kuhakikisha pointi tatu zinapatikana," amesema Zimbwe Jr.

Back to homepage
Share this story